Ukiona propaganda nyingi zinafanyika ili kujaribu kuzima utambulisho wa fundi kutoka Mali, Lassine Kouma hapo unapata jibu ni kwa kiasi gani nyota huyu kutua Yanga maumivu ni makali upande ule wa pili
Kwa misimu miwili mfululizo, Kouma ameingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Mali, akishinda tuzo hiyo msimu uliopita
Umri wake ni miaka 21, alikuwa nahodha wa Stade Mallien, msimu uliopita akihusika katika mabao 13, akifunga 7 na kutoa asisti 6
Jezi namba 8 aliyokabidhiwa itawakumbusha Yanga mbali sana kwani kabla ya ujio wa Khalid Aucho, jezi hiyo ilikuwa ikivaliwa na fundi Haruna Niyonzima
Huyu ndiye mrithi halisi wa Stephane Aziz Ki aliyetimkia Wydad Athletic, namba 10 imepata mchezaji kweli
Wananchi wanasema Kouma wanaye na wanatamba nae, Yanga imefanya usajili kweli...!