Msimu huu umekuwa mgumu, tumepambana kiume - Nadir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2018
Msimu huu umekuwa mgumu, tumepambana kiume - Nadir
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye amedumu katika kikosi cha Yanga kwa miaka 12 amekiri kwamba pengine wakati huu ndio mgumu kwa wachezaji kuliko wakati mwingine wowote aliowahi kukutana nao ndani ya klabu ya Yanga.

Nadir amesema mwaka huu wachezaji wa Yanga wamekutana na changamoto nyingi lakini akawasifu kwa upambanaji wao uliopelekea timu hiyo kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho licha ya kukosa ubingwa wa VPL msimu huu.

Katika mahojiano yake na mtandao wa Sport Xtra, Cannavaro amefunguka mambo mengi lakini kubwa ni kuelezea jinsi walivyofanikiwa kupambana mpaka wakati huu msimu unamalizika licha ya kukumbana na changamoto nyingi.

"Nimekuwa nikipata tabu sana kwa sababu mimi ndiye nawaangalia sana wachezaji wenzangu hasa katika kipindi hiki ambacho tunapita, ni kigumu sana.

Kila mwana Yanga anajua tunapita katika kipindi gani, lakini nawapongeza sana vijana wangu wamefanya kazi na wanastahili sifa.

Katika miaka yote niliyokaa Yanga, hawa vijana wanastahili sifa. Siwezi kutangaza masuala ya klabu yangu lakini vijana wanastahili sifa kwa sababu ni wastahimilivu.

Kuwarudisha kwenye mchezo inahitaji moyo sana unakaa na kuzungumza nao kinachosaidia ni kwamba wananisikiliza kila nikiwaambia kituna bado tunaendelea kupambama na timu yetu ili tuifikishe kwenye hali nzuri. Kwa sasa wachezaji wengi wanasumbuliwa na majeraha nikiwepo mimi mwenyewe.

Kwenye ligi tumekosa, sasa hivi macho yetu yapo kwenye Caf Confederation Cup kama tukiweza kupata nafasi hapa na kufika nusu fainali tunaweza kupatabupendeleo wa kuongeza timu tukapata nafasi ya kuingiza timu tatu hadi nne kwenye mashindano ya Afrika.

Nawaita wachezaji wazoefu tunajadili kwamba kitu fulani kina wezekana na vitu vingine haviwezekani nikimalizana na wachezaji wazoefu wale wengine vijana hawanisumbui naweza kuzungumza nao vizuri.

Hakuna mtu ambaue hajui Yanga imepita kwenye kipindi kigumu mwaka huu, nasikia fununu watu wanasema wachezaji wa Yanga tumegoma, hakuna mchezaji aliyegoma. Huu ni mpira wachezaji tunaendelea na mazoezi, najua kila mtanzania anajua Yanga tuna shida lakini sisi tunapambana hii ndiyo kazi yetu.

Sijaelewa kwa sababu kuna watu wanamaliza mikataba yao sijui viongozi watakaa vipi na wachezaji, mchezaji anapomaliza mkataba inakuwa nje ya uwezo wangu. Mtu akimaliza mkataba siwezi kuzungumza nae kwa sababu ni suala ambalo lipo nje ya mkataba wangu."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’