Yanga imemthibitisha Romain Folz kuwa Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa nchi akichukua nafasi iliyoachwa na Miloud Hamdi
Folz anatua Yanga akiwa na kibarua cha kuendeleza utamaduni wa kushinda mataji kwa Wananchi
Lakini kiu kubwa ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao inafanya vizuri zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Kocha huyo raia wa Ufaransa akiwa pia na asili ya Morocco, atakuwa na takribani wiki sita za kukiandaa kikosi chake kabla ya kukaribisha msimu mpya Septemba 2025
Karibu Jangwan Folz...
ADVERTISE HERE