Yanga imetambulisha usajili wa kiungo kinda Abdulnasir Mohammed 'Casemiro' kutoka klabu ya Mlandege, mabingwa wa ligi kuu ya Zanzibar
Ujio wa Casemiro mwenye umri wa miaka 20 ni mwendelezo wa Yanga kusajili wachezaji wenye vipaji vikubwa visiwani Zanzibar
Katika tuzo za Farafa Zanzibar msimu uliomalizika (2024/25), Casemiro alitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi baada ya kuiongoza Mlandege kutwaa taji la ligi kuu
Casemiro pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Zanzibar Heroes kilichotwaa michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu
Karibu Jangwani Casemiro...!
ADVERTISE HERE