Yanga kuanza na Thank You

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jul 2025
Yanga kuanza na Thank You

Klabu ya Yanga leo imepanga kuanza kutoa taarifa za maboresho ya kikosi ambapo itaanza na wachezaji ambao haitokuwa nao kwa msimu ujao wa mashindano.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amesema tayari amekabidhiwa faili la wachezaji wanaotakiwa kuondoka ili kupisha wachezaji wengine, watakaobaki na wale ambao wamesajiliwa kwa msimu uja

"Tayari nimepokea ripoti ya maboresho ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao. Ripoti imegawanyika, kuna wachezaji ambao mikataba yao imeisha, mwalimu kasema hawa tuwafungulie milango waende, pili kuna wachezaji ambao tumewaongeza mikataba, wapo tuliovunja nao mikataba na wale ambao tumewapa mikataba mipya"

"Kwa hiyo nikianza kutoa ripoti nitaanza kuchagua nianze wapi, nipige kwenye utosi, au nianze kupunguza watu," alisema Kamwe

Aidha Kamwe, amebainisha kuwa waliamua kumtambulisha mpema kiungo Moussa Balla Conte ili kuichangamsha nchi, huku akiwaambia mashabiki wa soka kuwa usajili wake wala si mkubwa kama wengi wanavyodhani, kwani wapo wengine zaidi yake

Katika wachezaji watakaoagwa ni pamoja na mshambuliaji Kennedy Musonda ambaye tayari ameelekea Israel baada ya mkataba wake kumalizika

Nyota wengine ambao huenda wasiwe sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao ni pamoja na Clatous Chama, Jonas Mkude, Farid Mussa, Aziz Andabwile, Khalid Aucho na Jonathan Ikangalombo ambaye huenda akatolewa kwa mkopo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
24m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’