Yanga kutangaza kocha mpya Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2025
Yanga kutangaza kocha mpya Jumatano

Klabu ya Yanga, wiki ijayo itamtambulisha kocha wake mpya ambaye anakwenda kuchukua mikoba iliyoachwa na Miloud Hamdi aliyejiunga na Ismailia baada ya kuingoza Yanga kutwaa mataji matatu kati ya matano ambayo Wananchi walitwaa msimu huu

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema taratibu zote kumuhusu kocha huyo zimekamilika na siku ya Jumatano au Alhamisi watamtangaza

"Maswali yamekuwa mengi na mashabiki wana shauku kubwa ya kutaka kumfahamu kocha wetu ni nani?"

"Sasa niwaambie mashabiki na Wanachama wa Yanga, siku ya Jumatano au Alhamis tutamtangaza kocha wetu mkuu," alisema Kamwe

Jina la aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Mamelodi Sundowns, Romain Folz ndio linatajwa zaidi kurithi mikoba ya Hamdi

Folz mwenye umri wa miaka 35 anarudi katika soka la ushindani baada ya msimu uliopita kuitumikia Olympique Akbou ya Algeria ambapo aliisaidia klabu hiyo kubaki ligi kuu katika mechi nane za mwisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’