Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu Yanga Ali Kamwe amedai siku ya Jumatatu atafika Mahakamani kula kiapo ili kubadili jina lake kutoka Ally na kuitwa Eliii
Upo msemo maarufu kwa wale waliosoma Cuba au wenye D mbili wanaweza kufahamu kile anachomaanisha Kamwe hasa ikizingatiwa ni kipindi cha usajili
Kuna mchezaji ambaye jina lake la kwanza linafanana na jina ambalo Kamwe anataka kubadili, ameomba kuvunja mkataba na waajiri wake wa sasa
Alijiunga nao dirisha dogo akisaini mkataba wa mwaka mmoja ambao baada ya kuutumikia kwa miezi sita, anaweza kuvunja
Baada ya usajili wa Moussa Balla Conte huku usajili wa mchezaji mwingine kutoka upande ule ukielekea kukamilika, Yanga inaweza tena kuokota embe dodo mchangani....
