Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube amezima propaganda zilizoanzishwa mitandaoni akiwahakikishia Wananchi yeye bado yupo sana
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dube ameandika ujumbe unaosomeka 'MAKOMBE YAENDELEE WANANCHI'
Mapema leo zilisambaa propaganda mitandaoni ziiizodai Dube ameishitaki klabu ya Yanga akidai fedha za usajili na alikuwa mbioni kuvunja mkataba na mabingwa hao wa nchi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alikanusha propaganda hizo na kusisitiza Yanga haina tatizo lolote na Dube
ADVERTISE HERE