Ni suala la muda tu Yanga itatambulisha usajili wa kiungo kinda Abdulnasir Mohammed 'Casemiro' anayetua kutoka klabu ya Mlandege, mabingwa wa ligi kuu ya Zanzibar
Katika tuzo za Farafa Zanzibar msimu uliomalizika (2024/25), Casemiro ametwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi baada ya kuiongoza Mlandege kutwaa taji la ligi kuu
Casemiro pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Zanzibar Heroes kilichotwaa michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amemtabiria kiungo huyo mkabaji kuwa atan'gara na kufanya makubwa katika klabu ya Yanga
Yanga pia imemnasa nyota mwingine chipukizi kutoka Zanzibar, beki kiraka Aboubakar Nidhar Otham 'Ninju' aliyekuwa akiitumikia JKU kwa mkopo akitokea Azam Fc
ADVERTISE HERE