Wiki chache zilizopita, Yanga ilikamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Celestine Ecua aliyekuwa akiitumikia Asec Mimosas kwa mkopo akitokea klabu ya Zoman Fc
Mapema wiki hii ukaibuka mvutano kati ya Ecua na kampuni inayomsimamia mchezaji huyo, WA FOOTBALL AGENCY juu ya usajili wake
Inaelezwa klabu moja ya Tanzania ilimalizana na wasimamizi wake kabla ya kufikia makubaliano na Ecua
Ecua akagoma kujiunga na timu hiyo akisisitiza yeye tayari amemalizana na Yanga na ndio klabu ambayo ataitumikia msimu ujao
WA FOOTBALL AGENCY wamemaliza utata sasa kwa kukubaliana na uamuzi wa mchezaji jana wakithibitisha Ecua kutua Yanga
"Baada ya mazungumzo marefu na mijadala ya kina, mchezaji wetu Ecua Celestin amesaini rasmi na Klabu ya Young Africans SC (Yanga SC)
Sura mpya inaanza katika moja ya vilabu maarufu zaidi Afrika Mashariki. Mkataba sasa umekamilika, na mchezaji atakuwa akisafiri kuelekea Tanzania hivi karibuni kujiunga na timu yake mpya.
Asante kwa pande zote zilizohusika katika kufanikisha uhamisho huu wa kiuadilifu. Tuendelee na changamoto mpya," taarifa ya kampuni hiyo ilithibitisha
Ni rasmi sasa, Ecua ni usajili uliokamilika kwa 100% akitarajiwa kutua nchini wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya pre-season