Aziz Ki alivyomleta Doumbia Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jul 2025
Aziz Ki alivyomleta Doumbia Yanga

Kiungo Mohammed Doumbia ambaye anatajwa kusajiliwa na Yanga katika dirisha hili, alikaa nje ya kiwanja kwa zaidi ya mwaka mmoja

Nyota huyo aliyewahi kuzitumikia FC Majestic ya Burkina Faso na Slovan Liberec ya Jamhuri ya Czech, alikuwa kwenye mgogoro na mkubwa na 'management' yake

Aliyefanikisha ujio wa kiungo huyo ni Stephanie Aziz Ki ambaye wakati yuko kwenye mchakato wa kujiunga na Wydad alimwambia Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kuhusu ubora wa Doumbia pamoja na kuwa amekaa nje ya uwanja kwa muda mrefu

Baada ya kupewa taarifa, Hersi akawasiliana na mchezaji na kuandaa taratibu za kumsafirisha kuja Dar es Salaam

Doumbia alipokelewa vizuri na kwa bahati nzuri alifika siku ambayo klabu ilikuwa na session ya mazoezi jioni katika uwanja wa Avic Town

Mchezaji huyo akapewa nafasi ya kufanya mazoezi na wenzake pale Avic Town, hadithi ya kusajiliwa kwake ikaanzia hapo

Uwezo aliokuwa akionyesha mazoezini sio tu ulimfurahisha aliyekuwa kocha wa Yanga wakati huo Miloud Hamdi bali hata wachezaji wenzake walivutiwa nae na hata kupendekeza asajiliwe

Doumbia ni kiungo kiraka ambaye anaweza kutumika katika eneo lolote kati yaani namba 6, 8 na hata namba 10

Doumbia anafananishwa na kiungo wa zamani wa Barcelona na Manchester City Yaya Toure, ana nguvu, kasi na maarifa anapokuwa na mpira mguuni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
27m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
35m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’