Yanga kukata wawili wa kigeni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2025
Yanga kukata wawili wa kigeni

Mpaka sasa ni wachezaji wawili wa kigeni ambao wamethibitishwa kuondoka Yanga na nafasi zao zitazibwa katika dirisha hili la usajili lililofunguliwa Julai 1

Mshambuliaji Kennedy Musonda tayari ametimkia Urusi huku Stephane Aziz Ki akijiunga na klabu ya Wydad CA ya Morocco

Katika wachezaji 12 wa kigeni ambao Yanga ilisajili msimu uliopita, nyota 10 bado wana nafasi ya kuendelea kuitumikia Yanga au kuachwa kwa kuzingatia mahitaji ya timu kuelekea msimu ujao

Mlinda lango Djigui Diarra, walinzi Chadrack Boka na Yao Kouassi, viungo Khalid Aucho, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Clatous Chama, Pacome Zouazoua na washambuliaji Prince Dube na Jonathan Ikangalombo

Diarra, Boka, Ikangalombo na Dube bado wana mikataba wakati Yao, Aucho, Duke, Maxi, Chama na Pacome mikataba yao imemalizika

Mpaka sasa taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imebainisha kuwa klabu tayari imewaongeza mikataba Pacome, Maxi, Aucho huku Duke nae akitarajiwa kusaini mkataba wakati wowote

Yao pia ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja lakini bado haijafahamika kama atajumuishwa katika usajili au la kwa kuwa bado ni majeruhi

Katika dirisha hili Yanga inaweza kuongeza wachezaji wanne hadi watano wa kigeni, ili kufanikisha italazimika kukata majina mawili ili kupata nafasi nne au majina matatu ili kupata nafasi tano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’