Mwandila aitaka Yanga ijipange, aeleza umuhimu wa kocha Mkuu kukaa kwenye benchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 May 2018
Mwandila aitaka Yanga ijipange, aeleza umuhimu wa kocha Mkuu kukaa kwenye benchi
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Noel Mwandila amesema kukosekana kwa kocha Mkuu kwenye benchi la ufundi huenda kukawa kumeigharimu Yanga kupata matokeo kwenye mchezo wa jana dhidi ya Rayon Sports.

Akizungumza baada ya mchezo wa jana ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Mwandila amesema licha ya kuwa walikuwa wakiwasiliana na kocha huyo aliyekuwa jukwaani wakati mchezo ukiendelea, lakini uwepo wake kwenye benchi ulihitajika zaidi.

Wengi wamekosoa mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi jana hasa kumtoa Kamusoko aliyekuwa akijitahidi kuichezesha timu.

Mwandila na Shedrack Nsajigwa ndio waliokaa kwenye benchi na mara kwa mara walionekana wakijadiliana juu ya nini kifanyike wakati mchezo ukiendelea.

Hakuna sababu zaidi iliyotolewa na uongozi wa Yanga zaidi ya kueleza kuwa kocha Mwinyi Zahera anasubiri kukamilika kwa vibali vyake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’