Musonda amemaliza mkataba Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2025
Musonda amemaliza mkataba Yanga

Mshambuliaji raia wa Zambia, Kennedy Musonda, yuko tayari kwa changamoto mpya baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, hatakuwa sehemu ya kikosi cha Wananchi msimu ujao.

Musonda aliyejiunga na Yanga SC akitokea klabu ya Power Dynamos ya Zambia, ameichezea timu hiyo kwa misimu miwili na nusu, akishiriki katika mafanikio makubwa ya kikosi hicho, ikiwemo kutwaa mataji ya ndani kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kombe la Shirikisho (CAF CC)

Hata hivyo, safari ya mshambuliaji huyo ndani ya Yanga imegubikwa na changamoto ya majeraha ya mara kwa mara, yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu msimu huu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na klabu, Musonda hakuweza kucheza katika mechi nyingi za msimu wa 2024/25, na alikosekana kabisa kwenye mechi za kuhitimisha msimu kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kiafya.

“Musonda amekuwa akisumbuliwa na majeraha kwa muda, jambo lililopunguza mchango wake kwa timu. Mkataba wake umeisha na tayari klabu imeamua kutomwongeza tena kwa msimu ujao,” kilisema chanzo

Hatua ya kutokuwepo kwake hata kwenye shamrashamra za paredi ya ubingwa iliyofanyika Jangwani Jumatatu imezidi kuzua maswali juu ya hatma yake kwani ni kama aliamua kujiondoa kikosini mapema

Tetesi kutoka vyanzo vya soka la Afrika Kaskazini zinadai kuwa Musonda yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Al Ittihad ya Libya, ambayo imeonyesha nia ya kumsajili kwa msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’