Nafikiri mpaka sasa hakupaswi kuwa na mjadala wa mchezaji gani anapaswa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu 'MVP'
Kwa sababu ni mchezaji mmoja tu ambaye anastahili tuzo hiyo, PACOME ZOUZOUA
Pacome jana amedhihirisha yeye ni mchezaji wa daraja la juu mwenye uwezo wa kuamua mechi kubwa
Alifunga bao la kwanza kupitia mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
Lakini pia akatoa pasi ya bao la pili kwa ufundi wa hali ya juu, Clement Mzize akapigilia msumari wa pili
Baada ya dakika 90 kukamilika, Pacome akabeba tuzo ya mchezaji bora wa mechi ikiwa ni tuzo yake ya nane msimu huu
Hakuna mchezaji mwenye tuzo nyingi za mchezaji bora wa mechi kumzidi

ADVERTISE HERE