Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu wa nne mfululizo
Yanga ilitwaa ubingwa jana baada ya kuwachapa watani zao Simba mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
"Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa 31 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ikiwa ni ubingwa wa nne mfululizo. Kwa zaidi ya miaka 85, upinzani wa Yanga na Simba umeendelea kuwa burudani kwa mamilioni ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Endeleeni kutupa burudani," ulisomeka ujumbe wa Rais katika kurasa za mitandao ya kijamii
Ulikuwa wa tano mfululizo kwa Yanga dhidi ya Simba na kuweka historia mpya ya vipigo baina ya timu hizo zenye upinzani wa kihistoria

ADVERTISE HERE