Yanga imetwaa taji la ligi kuu ya NBC kwa msimu wa nne mfululizo ikiichapa Simba mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ilikuwa mechi ya upande mmoja kwa muda mwingi katika kipindi cha pili Yanga ikiandikisha ushindi wake kupitia mabao ya Pacome Zouzoua aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari pia akitengeneza bao la pili lililofungwa na Clement Mzize
Ushindi huu wa leo ni heshima kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi na mashabiki wa Yanga hasa kwa kuzingatia 'mazingaombwe' yaliyogubika mchezo huo namba 184
Zile kelele mitaani ni wazi leo zimezimika kwa ushindi huu ambao sio tu unadhihirisha ubora wa Yanga, lakini ni ushindi wa heshima kwani wananchi walilazimika kupambana na mamlaka nje ya uwanja kuhakikisha haki hii inapatikana'


