Kessy ataka 'nyomi' uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2018
Kessy ataka 'nyomi' uwanja wa Taifa
Beki wa kulia wa Yanga Hassani Kessy amewataka mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria wa soka la Tanzania kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kesho Jumatano kuiunga mkono timu yao itakapokuwa inachuana na Rayon Sports katika mchezo wa pili wa kundi D kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kessy amesema wamejiandaa kikamilifu kupata matokeo kwenye mchezo huo lakini akasisitiza umuhimu wa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa 'mzuka'

"Unapoingia uwanjani na kukuta mashabiki wengi unapata nguvu ya ziada," amesema Kessy.

"Mchezo wa kesho ni muhimu sana kwetu kupata ushindi. Tunahitaji sapoti ya mashabiki."

Kessy ni miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa moja jioni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
36m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’