Matchday : Yanga vs Simba, NBC PL, Juni 25

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jun 2025
Matchday : Yanga vs Simba, NBC PL, Juni 25

Wanasema usiku wa deni haukawii, hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imefika. Ni mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa leo saa 11 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni mechi namba 184 ambayo awali ilipaswa kupigwa March 08 lakini haikufanyika baada ya Simba kugoma kucheza maamuzi ambayo yalipelekea Yanga kuweka msimamo wa kutocheza tena mechi hiyo hadi wale waliohusika kukwamisha dabi hiyo wachukuliwe hatua

Baada ya kilio cha Yanga kusikilizwa hatimaye Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mnguto na Mtendaji Mkuu Almas Kasongo wakan'goka katika Bodi ya ligi na Yanga kuridhia kucheza mchezo huo katika tarehe nyingine tofauti na Juni 15 ambayo Bodi hiyo ilikuwa imeupangia mchezo baada ya kuahirisha March 08

Mechi ya leo inakwenda kufunga hesabu za msimu huu, timu itakayoibuka na ushindi inakwenda kubeba taji la ligi kuu

Hivyo ni kama fainali lakini Wananchi wakiwa na faida zaidi kwani ushindi au hata matokeo ya sare yatawapa ubingwa. Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 79 huku watani zao Simba wakiwa na alama 78

Yanga imepata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo, ikianzia maandalizi yake visiwani Zanzibar na jana kuhitimisha katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Mashabiki wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuipa sapoti timu yao katika mchezo ambao Yanga haipaswi kupoteza ili kutwaa ubingwa

Kumekuwa na propaganda nyingi nje ya uwanja kutoka upande wa Simba lakini taarifa ya uhakika ni kuwa saa 11 jioni nyasi za dimba la Mkapa zitawaka moto wakati mafahari wawili wakichuana

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amewahakikishia Wananchi kuwa kikosi chake kiko tayari na wanakwenda kupambana ili kushinda mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’