Tshishimbi hatihati kuikabili Rayon Sports

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2018
Tshishimbi hatihati kuikabili Rayon Sports
Kiungo mahiri wa Yanga Papi Kabamba Tshishimbi huenda asiwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoikabili Rayon Sport kwenye mchezo wa pili wa kundi D, kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa kesho Jumatano, May 16.

Tshishimbi alipata majeraha katika mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya hatua ya makundi dhidi ya Wolaitta Dicha kisha kujitonesha kwenye mchezo dhidi ya Simba, alirejea kwao DR Congo kusaka tiba 'mbadala' ya majeraha yake.

Kuna taarifa kwamba Tshishimbi tayari emerejea jijini Dar es salaam lakini hakuna uhakika kama atacheza mchezo huo kwa kuwa hajafanya mazoezi na wenzake.

Tshishimbi hakuwa miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kuelekea mchezo huo.

Iwapo kiungo huyo mahiri atakosekana pamoja na Said Juma 'Makapu' anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano, huenda kiungo Patto Ngonyani ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichocheza michezo ya ligi dhidi ya Prisons na Mtibwa Sugar akachukua majukumu yao.

Kelvin Yondani na Obrey Chirwa nao wamerejea kikamilifu kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga kuelekea mchezo huo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
57m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’