Yanga yataka ushindi wa heshima dabi ya Kariakoo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2025
Yanga yataka ushindi wa heshima dabi ya Kariakoo

Kuelekea mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, klabu ya Yanga imeweka msimamo mkali: ushindi ni lazima!

Katika kikao kizito kilichofanyika jana Jumatatu kabla ya safari ya kurejea jijini Dar es Salaam, wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa juu wa klabu hiyo walikutana kwa ajili ya kuweka malengo ya mwisho kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Mechi hiyo, ambayo imeahirishwa mara mbili kutoka Machi 8 na Juni 15, sasa itapigwa kesho, Juni 25, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11 jioni. Ni mchezo unaobeba hatima ya ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu huu, ambapo Yanga inaongoza kwa alama moja dhidi ya watani wao Simba.

“Tumekutana na vijana tumewaambia maana halisi ya mchezo huu... huu si mchezo wa kawaida. Heshima ya viongozi wetu na mashabiki iko mezani, na kitu pekee tunachohitaji ni ushindi,” alisema mmoja wa mabosi wa Yanga.

Katika kikao hicho, wachezaji walipewa maagizo maalum ya kuhamasishana na kuweka akili zote kwenye mechi hiyo, ambayo huenda ikaamua bingwa wa msimu huu. Imeelezwa Mfadhili/Mdhaamini wa Yanga GSM ameweka mezani kitita kisichopungua Tsh Milioni 500 kwa ajili ya ushindi katika mchezo huo

Yanga, yenye pointi 79 baada ya mechi 29, haihitaji kupoteza mchezo huo ili kubeba taji. Simba wanafuatia kwa pointi 78, hivyo mechi hii ni fainali isiyo rasmi ya Ligi Kuu msimu wa 2024/25.

Kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar es Salaam jana mchana tayari kwa maandalizi ya mwisho. Baada ya kuwasili bandarini, timu ilielekea moja kwa moja kambini Avic Town, Kigamboni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’