Mwenyekiti wa zamani wa Yanga Dk Mshindi Msolla ni miongoni mwa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi utakaofanyika August 16 jijini Tanga
Licha ya kurejesha fomu ndani ya muda, Dk Msolla nae amelalamika kukosa udhamini kama ilivyokuwa kwa wagombea wengineΒ
Amesema anasubiri maamuzi ya Kamati ya uchaguzi na kama hataridhika basi atachukua hatua kwa kufuata taratibu zilizowekwa
"Baada ya Kamati ya uchaguzi kutangaza mchakato, niliamua kuchukua fomu kwa kuwa niliona nina sifa zinazotakiwa, nimecheza, nimefundisha na nimeongoza mpira"
"Nilitimiza wajibu wangu kwa kujaza fomu, nikalipa laki 5 lakini changamoto kubwa ambayo nimeipata ni kwamba sikupata fursa ya 'endorsement'"
"Kila nilipojaribu waliniambia kwamba hilo zoezi lilimalizika kipindi kirefu sasa kama tulipewa siku tano wote ilikuwaje mwenzetu apate endorsement ya kila sehemu?"
"Ukweli ni kwamba endorsement hizo zimefanyika nje ya kipindi cha uchaguzi hilo sio jambo sahihi. Kutopewa nafasi ya kupata mtu wa kukudhamini ni kosa, huu ni uhujumu"
"Mpira ni wa kila mtu sio mtu mmoja, ni kwamba sijaridhika na maamuzi yaliyofanyika na kiongozi ambaye yuko madarakani, kanuni inamruhusu awe na wadhamini angalau watano, sasa inakuwaje ana wadhamini 46? Lengo lake ni nini? kama yeye amefanya kazi yake vizuri alipaswa kutusubiri kwenye boksi la kura ili haki itendeke"
"Mimi binafsi nangojea kamati ya uchaguzi itakapotoa maamuzi yake kisha tutaangalia taratibu nyingine zinazofuata ili tupate haki yetu," alisema Dk Msolla