Tuzime TV, twendeni tukachukue ushindi uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2018
Tuzime TV, twendeni tukachukue ushindi uwanja wa Taifa
Yanga ina nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kama itafanya vizuri kwenye michezo mitatu ya nyumbani.

Mchezo wa Jumatano dhidi ya Rayon Sports ni moja ya michezo hiyo mitatu ambayo Yanga lazima ishinde.

Ushindi utapatikana kama mashabiki tutajitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kuiunga mkono timu yetu.

Huu ndio wakati ambao mashabiki wa Yanga wanapaswa kuwa karibu na timu yao pengine kuliko wakati mwingine wowote.

Kutojitokeza kwa wingi uwanjani kutapunguza zaidi morali ya wachezaji na kuwafanya wajihisi kama wako 'yatima'.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameweza kuirudisha Yanga katika hali ya ushindani na ameahidi kikosi chake kitawashangaza wengi kesho.

Kocha huyo asiye na mzaha awapo kazini, aligawa timu kwenye vikosi viwili, kimoja kikisafiri kucheza dhidi ya Prisons na Mtibwa Sugar na kingine akibaki nacho jijini Dar es salaam kukiandaa kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Jana wachezaji wote waliingia kambini na leo wanatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo utakaoanza saa moja jioni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’