Hamdi apania ushindi dhidi ya Dodoma Jiji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jun 2025
Hamdi apania ushindi dhidi ya Dodoma Jiji

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema hawana nafasi ya kufanya makosa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Hamdi amesema wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa

Hata hivyo amesisitiza mchezo hautakuwa mwepesi kwani kila timu inayocheza dhidi ya Yanga hupambana kwa kila namna kupata matokeo mazuri

"Mimi sitakuwa na maneno mengi kwa sababu mchezo dhidi ya Dodoma Jiji tunahitaji kushinda hatutaki kusikia sare au kupoteza"

"Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi kwa sababu kila timu inayocheza dhidi ya Yanga hupambana hadi tone la mwisho"

"Ni muhimu kwetu kushinda mchezo huu na tukifanikiwa nadhani tunaweza kuanza kufikiria ubingwa"

"Wachezaji wote wanafahamu jukumu lililoko mbele yao naamini watacheza kwa ari kubwa kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Hamdi

Akizungumzia hali ya kikosi, Hamdi amesema washambuliaji Prince Dube na Kennedy Musonda watakosekana lakini wachezaji wengine wote wapo

"Dube alipata majeraha madogo katika mchezo uliopita, tumekuja nae Zanzibar kwa ajili ya kuendelea kuimarisha afya yake, Musonda bado mgonjwa," aliongeza Hamdi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’