Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amekutana na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki pamoja na mchezaji mwenzake Selemani Mwalimu
Aziz Ki na Mwalimu wanlikutana na Hersi baada ya kumalizika kwa mchezo wa kombe la Dunia la klabu kati ya Wydad Athletic dhidi ya Manchester City
Ki amemshukuru Hersi kwa kuendelea kumuunga mkono:
"Kuona uko hapa na familia ukiniunga mkono kunanionyesha kuwa wewe si tu Rais, bali ni mtu mkubwa sana. Asante kwa kuwa ndiye uliyefungua mlango huu wa Tanzania kwangu, na hasa kwa msaada wako katika kila hatua ya maisha yangu"
"Asante kwa kunijali kama baba. Mungu akubariki na akulinde ili uendelee kuipeleka Yanga juu sana na mbali sana. Wananchi, jivunieni Rais wenu Hersi na kazi yote anayoifanya kwa ajili ya watu wetu," aliandika Aziz Ki katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii


