Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema mshambuliaji Prince Dube naendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya awali kufuatia majeraha aliyopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons jana
Etutu amesema Dube aliumia nyama za paja upande wa kushoto, wamebaini changamoto hiyo baada ya kumfanyia uchunguzi wa awali, amesema mchezaji huyo atafanyiwa vipimo zaidi jijini Dar es salaam siku ya IjumaaΒ
"Jana bahati mbaya akiwa anajiribu kuruka ili kuupiga kichwa alipata shida hiyo katika nyama za paja kwa uchunguzi tuliufanya nyama za pacha zimevutika kwa kiasi kikubwa hadi kumsababishia maumivu makali," amesema Dk Etutu na kuongeza;
"Tumemwanzishia matibabu ya hatua ya kwanza anaendelea vizuri na tunategemea ataanza vipimo zaidi tukirejea Dar es Salaam."
Etutu amesema vipimo zaidi vitakavyofanyika ndio vitatoa taswira ya jeraha alilolipata litamuweka nje ya uwanja kwa muda gani lakini akiwahakikishia Wananchi kuwa nyota huyo atarejea dimbani mapema
''Kwa sasa anaendelea vizuri na tumemfanyia matibabu ya awali ambayo hayategemei vipimo na anaonyesha kuwa katika hali nzuri tunategemea mambo yataenda vizuri atarejea kabla ya mechi zilizo mbele yetu," alisema
Kikosi cha Yanga kimeondoka mkoani Mbeya kurejea jijini Dar es salaam na wanatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar kumenyana Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu raundi ya 30 utakaopigwa New Amaan Complex, Jumapili Juni 22