Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema amekiandaa kikosi chake kikamilifu kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa kesho Jumatano, Juni 18 katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, amesema wachezaji wake wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na mechi nyingine tatu zitakazofuata ili kuhakikisha wanatetea mataji yao
"Tunakabiliwa na fainali nne kuanzia mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons. Ni lazima tushinde mechi hizi zote ili kutetea mataji yetu"
"Kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huu, tumejiandaa vyema kiufundi ili kuhakikisha tunaibuka na ushindi"
"Sijali upande wa wapinzani wetu wamejiandaa vipi kuelekea mchezo huo lakini sisi hatujaja hapa Mbeya kutembea, kumekuja kuchukua alama tatu, tuko sawasawa na hakuna matokeo mengine tunahitaji zaidi ya ushindi"
"Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwani tutacheza dhidi ya timu imara yenye uzoefu mkubwa na ligi ya Tanzania lakini niseme tu tumefanya aina ya maandalizi tunayohitaji ili kushinda mechi hii," alisema Hamdi
Katika mchezo huo Hamdi atamkosa mshambuliaji Kennedy Musonda aliyebaki jijini Dar es salaam akiwa mgonjwa
Hamdi amesema katika mechi hizi za kuhitimisha msimu alitamani kuona kila mchezaji anakuwa sehemu ya kikosi katika mapambano ya kuhakikisha alama tatu zinapatikana katika kila mchezo