Msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, klabu ya Al Hilal ilikuwa kundi A na Yanga na ilifanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuongoza kundi hilo lililokuwa n MC Alger, Yanga na TP Mazembe
Katika kikosi cha Al Hilal, jina la winga Jean Claude Girumugisha raia wa Burundi ndilo lililozungumzwa zaidi kutokana na kasi yake na umahiri wa kupiga mashuti makali akitokea winga ya kushoto ingawa anatumia mguu wa kulia
Katika mchezo wa mkondo pili ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 huko Mauritania baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam, beki Kibwana Shomari alilazimika kufanya kazi ya ziada kumdhibiti winga huyo aliyekuwa akitereza kama samaki majini
Sasa inaelezwa Yanga inampigia hesabu Kirumugisha aliyezaliwa Septemba 18, 2004 ili kumjumuisha katika kikosi chake kuelekea msimu ujao
Al Hila wako tayari kumuuza winga huyo lakini wanataka dau la usajili lisilopungua Bil 3 za Kitanzania. Bado Yanga haijawasilisha ofa yake rasmi ili kufungua mazungumzo ya kumnasa 'kiberenge' huyo
Yanga tayari imefanya biashara ya kumuuza kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki aliyetimkia Wydad Athletic huku kukiwa na taarifa ya kuwa mbioni kumuuza mshambuliaji Clement Mzize anayekwenda kujiunga na Zamalek ya Misri
Ni wazi Yanga itahitaji kuziba nafasi za wachezaji hao na sifa ya wachezaji watakaosajiliwa ni lazima waingie moja kwa moja katika kikosi cha kwanza
Girumugisha alijiunga na Al Hilal ya Sudan Septemba 28, 2023, akitokea Magara Young Boys ya kwao Burundi, ambapo amekuwa na kiwango kizuri cha kuzivutia timu mbalimbali, huku msimu huu akifunga mabao 12 na kuasisiti 11 akiwa na kikosi hicho.
Pia, ameiwezesha timu hiyo chini ya Kocha, Florent Ibenge, iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu ya Mauritania 'Ligue 1' msimu huu kutwaa ubingwa, baada ya kucheza mechi 30, ikishinda 20, sare saba na kupoteza mitatu, ikiongoza na pointi zake 67.