Pacome anaitaka tuzo ya MVP msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2025
Pacome anaitaka tuzo ya MVP msimu huu

Katika msimu wa 2024/25 wa Ligi Kuu ya NBC, jina la Pacome Zouzoua linazidi kung'aa kama moja ya vipenzi vya Wananchi na moja ya nyota walioweka alama kubwa ndani ya uwanja.

Kiungo mshambuliaji huyu wa Yanga SC anazidi kuthibitisha thamani yake si tu kama mchezaji bora wa kikosi chake, bali pia kama mgombea halali wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP).

Msimu wa takwimu zenye uzito

Zouzoua, aliyejiunga na Yanga akitokea ASEC Mimosas msimu wa 2022/23, ameendeleza ubora wake kila msimu. Hata hivyo, msimu huu umekuwa wa kipekee zaidi. Hadi sasa:

    Mechi: 23

  • Mabao: 9

  • Asisti: 8

  • Ushiriki wa jumla katika mabao: 17

Kwa kulinganisha, msimu uliopita alihusika katika mabao 11 tu (mabao 7, asisti 4) ndani ya mechi 23. Hii inaonyesha wazi kuwa ameongezeka kiutendaji, na amekua kuwa kiungo hatari zaidi mbele ya lango.

Bado mechi tatu, nafasi ya kuthibitisha ubora

Yanga bado ina mechi tatu muhimu dhidi ya:

  • Tanzania Prisons (Juni 18)

  • Dodoma Jiji (Juni 22)

  • Simba SC (Juni 25)

Kwa Pacome, hii ni nafasi adhimu kuongeza takwimu zake na kuimarisha nafasi yake katika kinyang’anyiro cha MVP. Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba yuko fiti baada ya kupona majeraha, na sasa anarudi uwanjani akiwa na njaa ya mafanikio zaidi.

Pamoja na ushindani mkali kutoka kwa mshambuliaji Prince Dube ambaye ndiye aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi katika kikosi cha Yanga (mabao 13, asisti 8 – jumla ya ushiriki kwenye mabao 21), Pacome anapaswa kuingia katika kinyang'nyiro cha tuzo hiyo kwa sababu;

  • Anafanya kazi katika nafasi ya kiungo – si rahisi kufunga na kutoa asisti kwa wingi kutoka eneo hilo

  • Ni mchezaji wa mechi kubwa – huibeba timu katika nyakati muhimu

  • Ana mchango mkubwa si tu katika takwimu, bali pia katika muunganiko na falsafa ya uchezaji ya Yanga

Katika misimu mitatu iliyopita Yanga ilibeba tuzo ya MVP kupitia kwa wachezaji Yannick Bangala, Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki

Msimu huu pia ina nafasi ya kubeba tuzo hiyo endapo itafanikiwa kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’