Kutoka mgogoro hadi maridhiano: Bodi ya Ligi kupitia mageuzi ya kihistoria

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
16 Jun 2025
Kutoka mgogoro hadi maridhiano: Bodi ya Ligi kupitia mageuzi ya kihistoria

Tarehe 7 Machi 2025, nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, kulitokea mvutano usiotarajiwa kati ya klabu ya Simba na wasimamizi wa uwanja huo. Simba walikuwa wamefika kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya  watani wao wa jadi, Yanga SC.

Tukio hili lilianza kama mvutano wa kawaida, lakini baadaye likageuka kuwa kisiki kikubwa cha kuibua mjadala mpana kuhusu uendeshaji wa ligi nchini Tanzania.

Kilichofuata kilikuwa mfululizo wa matukio yaliyoitikisa soka la Tanzania. Simba waliondoka bila kufanya mazoezi na baadaye usiku waliandika barua wakieleza kutoshiriki mchezo huo, wakilalamikia kile walichokiita "kuingiliwa na mabaunsa wa Yanga".

Hata hivyo, wengi waliona sababu hiyo haina uzito wa kutosha kuhalalisha kugomea mechi, hasa mechi kubwa kama hiyo.

Uamuzi wa Kushtua

Licha ya tamko la Bodi ya Ligi kuwa mchezo ungeendelea kama ulivyopangwa Machi 8, hali ilibadilika ghafla. Ilipofika saa 8 mchana siku ya mechi, Bodi ya Ligi ilitangaza kuahirisha mchezo huo, na kuwaacha wadau wa soka nchini wakiwa na mshangao mkubwa.

Yanga, kwa upande wao, walifuata taratibu zote, wakafika uwanjani tayari kwa mchezo, lakini walijikuta wakikosa maafisa wa kusimamia mchezo.

Malalamiko ya Yanga na Safari ya Haki

Yanga haikusita. Ilitoa tamko la kupinga uamuzi wa kuahirisha mchezo na kutaka viongozi wa juu wa Bodi na TFF kujiuzulu. Walipokosa majibu, wakaamua kupeleka malalamiko yao katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Ingawa CAS haikusikiliza kesi hiyo moja kwa moja, ilirudisha shauri hilo kwa mamlaka za ndani kama hatua ya kwanza ya kutafuta suluhu.

Yanga, wakiwa na wasiwasi kuhusu haki kupatikana kupitia TFF, wakakimbilia Baraza la Michezo la Taifa (BMT). Hatua hii ilisababisha kuitishwa kwa mkutano wa maridhiano kati ya Yanga na Bodi ya Ligi, ambapo Yanga walisisitiza kutocheza hadi hatua madhubuti zichukuliwe.

Ushindi wa Mpira – Mabadiliko ya Viongozi

Mjadala huu hatimaye ulifika mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, ambapo pande zote ziliitwa na kusikilizwa. Hatua zilizochukuliwa baada ya hapo zilithibitisha kuwa Yanga walikuwa na hoja za msingi.

  • Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, alijiuzulu.

  • Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi, Almas Kasongo, alifutwa kazi na Rais wa TFF, Wallace Karia.

  • Ratiba ya mchezo namba 184 kubadilishwa kutoka Juni 15 hadi Juni 25

Mabadiliko haya hayakuwa kwa faida ya Yanga pekee, bali yanaleta matumaini kwa kila timu inayoshiriki ligi kuu. Kwa muda mrefu, baadhi ya vilabu vilijiona vikiwa wahanga wa maamuzi yasiyo na haki, lakini sasa mwanga umeonekana.

Bodi Huru ya Ligi – Tumaini Jipya

Pendekezo la kufanya Bodi ya Ligi kuwa chombo huru limepongezwa na wadau wengi. Mara nyingi migogoro ya soka nchini imekuwa ikichochewa na mgongano wa kimaslahi kati ya Bodi ya Ligi na TFF. Kwa bodi huru, taratibu zitafuatwa kwa haki, uwazi na bila upendeleo jambo linalohitajika sana katika kukuza heshima ya ligi yetu.

Huu si ushindi wa Yanga pekee, ni ushindi wa mpira wa miguu Tanzania. Ni ushindi wa uwazi, utawala bora na uongozi wenye kuwajibika. Mabadiliko haya yawe mwanzo wa enzi mpya ya soka la Tanzania ambako haki, uwajibikaji na hadhi ya mchezo vitatangulizwa mbele ya kila kitu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’