Kauli ya Lwandamina kuhusu mazoezi anayompa Ajib

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
30 Jul 2017
Kauli ya Lwandamina kuhusu mazoezi anayompa Ajib
Hakuna shaka kuwa mshambuliaji Ibrahim Ajib anaingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Mwalimu George Lwandamina baada ya kumpagawisha Mzambia huyo.

Licha ya kufanya mazoezi mengine ya kikosi, Lwandamina amemwandalia Ajib mazoezi yake binafsi ili kumuimarisha zaidi.

Aidha, Lwandamina amefunguka kuwa Ajibu ni mshambuliaji anayemtegemea kwenye safu yake ya ushambuliaji hivyo ni lazima amuandae ili aweze kucheza kwa mifumo anayohitaji yeye.

"Ni mchezaji mwenye kipaji na nimeamua kumpa mazoezi binfsi ili aweze kusaidiana na Donald Ngoma kwenye kikosi changu cha kwanza msimu ujao,"amesema Lwandamina.

Mzambia huyo amesema pamoja na kumpa mazoezi hayo Ajibu, lakini bado timu yake haijawa na kikosi cha kwanza cha kudumu hivyo niwajibu wa kila mchezaji kucheza kwa bidii kwenye mazoezi ili kumshawishi aweze kumpa nafasi.

Jamani jamani, hii safu ya ushambuliaji ya Yanga inaogofya, timu zijipange kwelikweli.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’