Sakata la madai ya fedha kati ya Yanga SC na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limechukua sura mpya baada ya uongozi wa Yanga kuwasilisha rasmi barua yenye vielelezo kadhaa kwa TFF leo, wakieleza kwa kina kile wanachodai na masharti ya namna ya kulipwa.
Ujumbe wa Yanga ukiongozwa na Mtendaji Mkuu, Andre Mtine, na Mkurugenzi wa Fedha, umefika ofisi za TFF na kuwasilisha barua rasmi yenye nyaraka na INVOICE takribani tano, huku wakisisitiza hawana tatizo na kudai au kudaiwa ilimradi kila kitu kifanyike kwa mfumo rasmi, unaozingatia uwazi na sheria.
Hivi Ndivyo Yanga Walivyopangilia Madai Yao kwa TFF:
1. Invoice za Ubingwa wa Federation Cup:
Yanga wamewasilisha invoice tatu za malipo wanayodaiwa kwa kutwaa Kombe la FA (CRDB) kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia msimu wa 2021/22. Haya ndiyo madai makuu yaliyoibua sintofahamu kubwa katika wiki za karibuni.
2. Mapato ya Mlangoni CAF:
Wamedai pia fedha za mapato ya milangoni kutoka mechi zao za michuano ya kimataifa (CAF), ambazo zilikatwa na CAF lakini TFF haijawasilisha sehemu ya mapato hayo kama inavyotakiwa kwa mujibu wa taratibu.
3. Udhamini wa Timu ya Wanawake na Vijana:
Pia wamesilisha madai ya fedha za udhamini kwa timu ya wanawake na mashindano ya vijana β maeneo ambayo mara nyingi hayajapewa kipaumbele lakini Yanga wameamua kuhakikisha kila senti inahesabiwa.
Machaguo Mawili kwa TFF kutoka Yanga:
Katika barua hiyo, Yanga wameipa TFF njia mbili za kufikia suluhu:
Chaguo la Kwanza:
-
TFF waweke fedha zote ambazo Yanga wanawadai (zinazokadiriwa kufikia Tsh Milioni 426).
-
Baada ya hapo, TFF watume INVOICE za madeni yao yote kwa Yanga.
-
Kisha Yanga wako tayari kulipa hayo madeni rasmi.
Chaguo la Pili:
-
Kama TFF tayari waliwakata fedha wanazodaiwa kutoka kwa Yanga, basi:
-
Watoe ushahidi wa malipo kwa risiti halali, kama inavyotakiwa kisheria kupitia sheria za kodi za Tanzania.
-
Baki ya fedha ya Yanga iingizwe moja kwa moja kwenye akaunti ya klabu.
-
Msimamo wa Yanga: Hakuna Maongezi Isipokuwa...
Yanga wametangaza msimamo usioyumba: Hakuna maongezi ya kawaida ya madeni (reconciliation) kwa njia isiyo rasmi.
βKama kuna haja ya kufanya mazungumzo, basi yafanyike mbele ya mamlaka rasmi kama vile TRA na vyombo vya usalama ili kumbukumbu ziwekwe sawa kisheria.β
Hii ni kauli nzito inayotilia mkazo umuhimu wa uwazi wa kifedha, na inalenga kulazimisha TFF kuwajibika kwa kila hatua waliyochukua kuhusu fedha zinazohusu vilabu.