Wakala amchelesha Mzize kutua Zamalek

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2025
Wakala amchelesha Mzize kutua Zamalek

Mpango wa mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, kujiunga na miamba ya soka ya Misri, Zamalek SC, umeingia dosari dakika za lala salama kufuatia mvutano kutoka upande wa wakala wa mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya duru za usajili, Yanga na Zamalek walikuwa wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo kuhusu uhamisho wa Mzize. Klabu hizo mbili zimekuwa zikijadiliana kwa wiki kadhaa na tayari walikuwa wameafikiana juu ya dau la usajili.

Hata hivyo, mambo yamekwama ghafla baada ya wakala wa Mzize, Jasmine Razack, kudai masharti ya ziada yanayodaiwa kuwa nje ya mipaka ya makubaliano ya awali. Zamalek wameamua kusitisha mchakato wa usajili kwa muda hadi sintofahamu hiyo itakapopatiwa ufumbuzi.

Jasmine Razack si jina geni katika mijadala ya soka ya Tanzania. Ametajwa mara kadhaa kuwa na mvutano na klabu ya Yanga, licha ya kuwahi kuwasimamia wachezaji kadhaa waliowahi kuichezea timu hiyo kama Fiston Mayele, Feisal "Fei Toto" Salum, na Jean Baleke – ambaye hata hivyo alilazimika kuachana na wakala huyo ili kuhitimisha uhamisho wake kwenda Jangwani.

Mzize, mwenye umri wa miaka 21, ameonyesha kiwango kizuri msimu huu, hali iliyowavutia vigogo mbalimbali wa Afrika. Yanga, ingawa bado ina mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo, imekuwa wazi kuhusu utayari wake wa kupokea ofa zinazomfaa mchezaji na klabu pia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’