Wakati uongozi wa Yanga ukitangaza msimamo wake kabla ya kukubali kucheza mechi namba 184 dhidi ya Simba kama Kamati ya saa 72 itavunjwa, CEO Bodi ya ligi na Katibu Mkuu wa TFF watajiuzulu, Kocha Miloud Hamdi yeye anaendelea kukiandaa kikosi chake KMC Complex kuelekea mechi za kuhitimisha msimu
Maandalizi ya kikosi hayajasimama kwani kama masharti yote yatakamilishwa, Yanga imeweka wazi itacheza dhidi ya Simba katika tarehe nyingine yoyote itakayopangwa
Lakini pia Yanga itacheza mechi nyingine mbili za ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji na endapo watalipwa fedha za ubingwa wa msimu uliopita kombe la CRDB, watacheza fainali ya msimu huu dhidi ya Singida Black Stars



ADVERTISE HERE