Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Mali Tom Saintfiet anatajwa kuhusika katika kumshawishi mlinda lango Djigui Diarra kuendelea kusalia katika kikosi cha Yanga
Yanga imepokea ofa nyingi kwa ajili ya Diarra lakini inaelezwa mlinda lango huyo namba moja wa Yanga na timu ya Taifa ya Mali ameuambia uongozi kuwa hataki kuondoka
Ushawishi wa Saintfiet aliyewahi kuinoa Yanga mwaka 2012, umetokana na mahitaji ya kocha huyo katika kikosi chake cha timu ya Taifa na umuhimu wa Diarra kusalia katika kiwango bora hasa ikizingatiwa kwa sasa ni mlinda lango tegemeo timu ya Taifa ya MaliΒ
"Nilisikia Diarra anataka kuondoka Yanga, nimekutana naye na nikamsikiliza kwenye hilo, kuna mambo nimemshauri anatakiwa kuyatazama kwa akili kubwa,β Saintfiet alinukuliwa na Mwanaspoti
"Nafahamu Diarra hawezi kukosa timu nzuri lakini timu alizonitajia zinazomtaka nadhani ni vyema akabaki Yanga kwanza kwa kuwa sioni kama sio sehemu sahihi kwake"
"Zipo timu ambazo zinaweza kukupa fedha nyingi lakini kwa hali ya vikosi vyao zinaweza kufifisha jina lake na hata kupoteza nafasi yake timu ya taifa, naona Yanga wamebadilika sana na wana njaa ya mataji makubwa ya Afrika, nadhani bado yupo sehemu sahihi"
Diarra yuko katika kikosi cha Yanga huu ukiwa msimu wa nne, ameendelea kuwa nguzo muhimu katika eneo la golikipa
Kipa huyo aliyetua Yanga Agosti 8, 2021 akitokea Stade Malien ya Mali, bado ana miaka miwili katika mkataba wake