Arafat kuongoza kikao na Bodi ya Ligi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jun 2025
Arafat kuongoza kikao na Bodi ya Ligi

Klabu ya Yanga leo itashiriki kikao maalum kilichoitishwa na Bodi ya ligi (TPLB) ili kutafuta mwafaka wa mchezo namba 184 ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao umepangwa kuchezwa Juni 15 huku Yanga ikigoma kushiriki mchezo huo

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Alex Ngai amethibitisha klabu kuitikia wito huo licha ya kuwa hawafahamu ajenda yake

"Ni kweli klabu ilipokea wito kutoka Bodi ya ligi kushiriki Mkutano huo ambao hatujataarifiwa ajenda yake ni ipi"

"Sisi ni klabu ya mpira, pamoja na kuwa viongozi wetu wengi wamesafiri, tumekubaliana wale waliopo watashiriki mkutano huo"

"Kwa sasa sina maelezo zaidi nafikiri tusubiri tumalize kikao, tutatoa taarifa kwa Wanachama na Mashabiki wetu juu ya kile kitakachojiri," alisema Ngai

Nae Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema msimamo wa klabu uko wazi, wanachotaka kuona ni kufanyiwa kazi kwa malalamiko yao kabla ya kukubali kushiriki mchezo huo

"Yanga ni klabu ya mpira wakiwa tayari kufanyia kazi matakwa yetu tutacheza, " alisema Kamwe

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji ataongoza viongozi wa Yanga huku Mtendaji Mkuu Andre Mtine, Wajumbe EXCom Rodgers Gumbo, Alex Ngai, Mwanasheria wa klabu na Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe

Akihojiwa na chombo kimoja cha habari, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto amewataka wadau wa soka nchini kuwaombea dua ili waweze kumaliza mgogoro huo salama kwa maslahi ya mpira wa miguu nchini

"Ni kweli tuna kikao leo, Watanzania waombee tu hili suala liishe salama kila upande uwe umeshinda, Sala zenu ndiyo zinahitajika," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’