Kitendo cha kocha wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje kumuweka nje kipa Ramadhani Kabwili kimekosolewa na mashabiki wengi wa soka nchini baada ya Heroes kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Mali kwenye uwanja wa Taifa.
Wengi wanaamini Ninje aliamua kumuweka nje Kabwili ili 'kumkomoa' baada ya sintofahamu iliyotokea baina yao kufuatia Kabwili kusafiri na Yanga nchini Algeria kushiriki mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger.
Ninje alimuondoa Kabwili kikosini kabla Rais wa TFF Wallace Karia hajaingilia kati na kumrejesha kipa huyo mwenye uzoefu wa michuano ya soka ya vijana.
Kabwili amekuwa kipa namba moja wa kikosi cha Ngorongoro Heroes tangu walipokuwa chini ya umri wa miaka 17 na aliiongoza timu hiyo kucheza fainali za AFCON mwaka jana nchini Gambia.
Ngorongoro Heroes imejiweka kwenye nafasi ngumu ya kutinga fainali za AFCON za vijana chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani huko Niger baada ya kipigo kutoka kwa Mali uwanja wa Taifa jana.
Heroes itahitaji kushinda mabao 2-0 ugenini ili kuweza kufuzu.

ADVERTISE HERE