Wanachama wa klabu ya Yanga wamewataka viongozi wa klabu hiyo kutojihusisha na mchezo namba 184 ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao umepangwa kupigwa Juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Wakizungumza katika mkutano uliofanyika makao makuu ya Yanga, Jangwni mapema leo, viongozi wa Matawi ya Yanga jijini Dar es salaam na mikoa ya jirani, wamesisitiza msimamo wa klabu hiyo huku wakiitaka Bodi ya ligi kutoka hadharani kueleza UMMA sababu zilizopelekea waahirishe mchezo wa kwanza uliopaswa kupigwa March 08
"Tunamwagiza mtendaji Mkuu wa klabu, awaambie maafisa wake wasije wakafanya kikao chochote kinachohusu mechi namba 184. Na viongozi wa kamati ya utendaji walilianzisha wao na sisi tukaliunga mkono, sasa atakayethubutu kupeleka timu yetu uwanjani tarehe 15, mlango uko wazi"
"Hatutanii wala hatufanyi maigizo, tuko tayari kwa adhabu yoyote ambayo wataona inafaa kwetu. Kwa hiyo kiongozi yeyote ambaye anaona ni vyema kupeleka timu tarehe 15 mlango uko wazi kuanzia Injinia na viongozi wengine wote mlango uko wazi"
Viongozi hao wa Matawi wamewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kutoingia katika propaganda zozote kwani msimamo wa klabu uko wazi, hakuna mechi Juni 15
"Tumemsikia msemaji wa Bodi ya ligi akieleza kuwa taratibu zote zinaendelea na mechi ya tarehe 15 ipo kama ilivyokuwa imepangwa. Sisi kama viongozi wa Matawi kwa niaba ya wanachama wetu tunaendelea kuunga mkono msimamo wa Kamati yetu ya utendaji, kuwa mechi namba 184 haitachezwa mpaka kile ambacho klabu yetu kimeainisha kwenye barua yetu ya March 09 tupate majibu yake"
"Wao wanatupangia mechi ya dabi tarehe 15 mwezi huu hatujapata majibu ya kile walichokuwa wanakifanyia uchunguzi, kwa hiyo sisi kama viongozi wa Matawi kwa niaba ya Wanachama tunasema hili hawatutendei haki na hatutapeleka timu uwanjani tarehe 15 mwezi huu"
"Kwa kuwa mechi haipo, tunawaomba wanachama na mashabiki wa Yanga walioko katika mikoa mbalimbali na hata Dar es salaam, wasihangaike na mechi ya terehe 15 kwani haipo," alisema Shabani Omary Mgonja, Mratibu wa Matawi ya Klabu ya Yanga mkoa wa Dar es Salaam
Nae Mratibu wa baraza la wazee ,Mzee Msumi amewataka mashabiki wa klabu Yanga kutofika Kwenye mchezo dabi Kariakoo utapangiwa tarehe 15 June kwenye dimba la Benjamin mkapa. Amesema wao kama klabu bado msimamo wao upo pale pale akiwata wananchi kujikita kwenye uchanguzi mkuu