TPLB ikiikata Yanga alama 15, itapaswa kujibu maswali haya

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
3 Jun 2025
TPLB ikiikata Yanga alama 15, itapaswa kujibu maswali haya

Bado kuna sintifahamu kubwa juu ya mchezo namba 184 kati ya Yanga SC na Simba SC uliopangwa kuchezwa tarehe 15 Juni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Licha ya nguvu kubwa kutumika kutangaza mchezo huo, bado kuna maswali ya msingi hayajajibiwa baada ya kutofanyika kwa mchezo huo March 08

Msimamo wa Yanga SC uko wazi: hawatacheza mchezo huo. Sababu yao kuu? Mchezo huo ulipaswa kuchezwa tarehe 8 Machi lakini haukufanyika, na hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya Simba, waliodaiwa kugomea mchezo huo, wala sababu rasmi za kuahirishwa hazijawahi kuwekwa wazi na TPLB.

Je, TPLB Ipo Tayari Kujibu Maswali Haya?

Ikiwa TPLB itaamua kuwapa Simba alama 3 na kuiadhibu Yanga kwa kupokonywa alama 15, kuna maswali magumu itapaswa kuyajibu:

  1. Kwa nini Simba hawakuchukuliwa hatua Machi 8?
    Kama kweli kanuni zinatoa adhabu kwa timu inayoshindwa kufika uwanjani, kwa nini zilikosa meno pale Simba walipogomea mechi ya Machi 8?

  2. Sababu halisi ya kuahirishwa kwa mechi ni ipi?
    Hadi sasa, TPLB haijaweka hadharani sababu ya kuahirishwa kwa mechi ya awali. Uwazi huu ni muhimu kabla ya kuchukua hatua dhidi ya klabu yoyote.

  3. Kwanini Azam Media inatangaza mechi ya Juni 15 huku Yanga wakiwa wamepinga?
    Ni sahihi kweli kuanza kutangaza mechi ambayo upande mmoja umeshatangaza hautashiriki? Je, hii si kuongeza mgogoro bila majibu ya msingi?

  4. Je, kanuni zitatumika kwa usawa?
    Ikiwa Simba hawakuadhibiwa kwa kutofika Machi 8, kwa nini Yanga waadhibiwe kwa kutofika Juni 15?

Hili sio tishio la alama pekee, ni kuhusu uhalali

Yanga wanasema wazi: hawakubali mchezo huo uchezwe pasipo majibu ya nini kilitokea awali. Kesi hii imeingia katika eneo la mgogoro wa uaminifu kati ya wadau wa soka na wasimamizi wa ligi.

Na kwa upande wa mashabiki, huu ni mtihani wa uadilifu wa TPLB, watasimamia kanuni kwa uweledi na usawa, au wataonekana kutekeleza shinikizo?

Kwa mujibu wa kanuni, iwapo timu itagoma kufika uwanjani bila sababu halali, inapoteza mechi na inaweza kupokonywa alama 15. Lakini hiyo hiyo kanuni, iliwapa Simba wajibu wa kufika uwanjani Machi 8 jambo ambalo hawakulitimiza.

Hivyo, endapo TPLB itaamua kuiadhibu Yanga peke yao, bila kurejea yaliyojiri awali, watafungua mlango wa malalamiko makubwa zaidi, na hata uwezekano wa kesi kurudishwa tena CAS/FIFA.

Hii kesi ya mechi ya Yanga dhidi ya Simba haipo tu juu ya ratiba, ipo juu ya kanuni kutekelezwa kwa haki na usawa. TPLB, kama taasisi inayoendesha ligi, inakabiliwa na jaribio kubwa la uaminifu. Ikiamua kuiadhibu Yanga, basi lazima kwanza ijieleze kwa kina kwa nini Simba hawakupata adhabu Machi 8.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’