Wazee Yanga wamjibu Mguto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2025
Wazee Yanga wamjibu Mguto

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Yanga Mohamed Msumi amejibu kauli ya Mwenyekiti wa Bodi ya ligi, Steven Mguto aliyesema kuwa mechi ya namba 184 kati ya Yanga dhidi ya Simba iliyopangwa kupigwa June 15 iko pale pale

Juzi akizungumza na wanahabari baada ya mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Singida BS, Mguto alisema bodi tayari imetangaza tarehe ya mchezo huo na hivyo hawayumbishwi na kauli zinazotolewa na viongozi wa Yanga kuwa Hawachezi

Mzee Msumi amesema bado bodi haijajibu madai yote yaliyotolewa na Yanga hivyo msimamo wao Wazee uko palepale, hawataruhusu viongozi wa Yanga kupeleka timu uwanjani

"Mpaka sasa bodi ya Ligi haijajitokeza hadharani na kujibu kwanza hoja tatu za Yanga, hivyo haitawezekana kwa wazee wa klabu kukubaliana na uamuzi wowote"

"Kwanza hatumtambui Steven Mguto kuwa mwenyekiti wa bodi ya ligi kwakuwa alishapoteza uhalali , kwani Mguto anawakilisha klabu gani ? Coastal Union tayari wana Mwenyekiti wao sasa yeye anawakilisha klabu gani?," alihoji Mzee Msumi

Katika miongoni mwa hoja zilizotolewa na Yanga, waliitaka Bodi ya ligi kuelezea sababu zilizopelekea waahirishe mchezo huo uliopaswa kupigwa March 08. Taarifa yao ya awali ilieleza wanachunguza mambo mbalimbali lakini badala yake Bodi imeupangia mchezo huo tarehe mpya bila kutoa majibu ya uchunguzi wao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’