Mlinda lango wa Yanga SC na timu ya taifa ya Mali, Djigui Diarra, ameendelea kutikisa anga za soka la Afrika baada ya kutajwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya Kipa Bora wa Afrika Magharibi kupitia CIS Awards 2025.
Diarra, ambaye amekuwa nguzo muhimu ya Yanga na timu ya Taifa ya Mali, anachuana na walinda lango wa ukanda huo waliofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika
Katika kinyang’anyiro hicho, Diarra atachuana na:
-
Edouard Mendy, mlinda mlango wa Al Ahli (Saudi Arabia) na aliyewahi kung’ara na Chelsea FC ya Uingereza
-
Youssouf Koita kutoka Djoliba FC (Mali)
-
Yaya Fofana wa Angers FC (Ufaransa)
-
Moussa Camara wa Simba SC (Tanzania)
Tuzo za CIS Awards, ambazo hutolewa kila mwaka, zinalenga kuonyesha na kuheshimu vipaji vya kipekee na ufanisi wa wanasoka kutoka ukanda wa Afrika Magharibi.