Yanga kumshusha Keita Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 May 2025
Yanga kumshusha Keita Dar

Klabu ya Yanga SC ya Tanzania inaonekana kuwa katika hatua za mwisho za kumalizana na mlinzi wa kulia wa TP Mazembe, Ibrahim Keita, ambaye yupo mbioni kutua jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo ya mwisho kabla ya kusaini mkataba, imefahamika.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti, Keita anatarajiwa kuwasili nchini Juni 12 kwa ajili ya kukamilisha dili hilo. Yanga imemfuatilia beki huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye amecheza kwa mafanikio ndani ya kikosi cha TP Mazembe kwa kipindi cha misimu mitatu, na sasa yupo ukingoni mwa mkataba wake na klabu hiyo ya DR Congo.

Hatua hii imechukuliwa na Yanga kwa ajili ya kuziba pengo la Yao Kouassi, ambaye anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Kouassi ni mmoja wa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Yanga, lakini jeraha lake limelazimu mabingwa hao wa Tanzania kuanza mipango ya kumtafuta mbadala wake mapema.

Keita amethibitisha kufanya mazungumzo na Yanga lakini akaweka wazi kuwa bado hawajafikia makubaliano ya mwisho.

“Ni kweli nimefanya mazungumzo na Yanga, lakini bado hatujafikia makubaliano. Nilikiona kikosi chao katika michuano ya kimataifa – ni timu nzuri. Kwa sasa namalizia mkataba wangu, lakini misimu mitatu ni mingi kucheza timu moja, mipango yangu ni kutafuta changamoto mpya,” alisema Keita.

Endapo dili hilo litakamilika, Keita atakuwa miongoni mwa usajili wa kimkakati wa Yanga kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa, hususan ikizingatiwa pengo litakaloachwa na Kouassi ambaye huenda asijumuishwe kwenye usajili hadi Januari 2026 – dirisha dogo litakapofunguliwa.

Yanga imeendelea kuwa klabu zenye mipango madhubuti ya kiufundi, na endapo Keita atasaini, basi atazidi kuimarisha eneo la walinzi wa pembeni akiungana na Israel Mwenda, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage na Chadrack Boka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’