Nabi yuko Dar, ana jambo na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
28 May 2025
Nabi yuko Dar, ana jambo na Yanga

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi, ametua nchini kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, lakini ujio wake hauishii tu kwenye mapumziko—kuna harufu ya mazungumzo mazito na uongozi wa Yanga.

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Nabi anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, huku lengo kuu likiwa ni kuzungumzia uwezekano wa kuwasajili nyota wawili wa klabu hiyo: kipa mahiri Djigui Diarra na mshambuliaji chipukizi Clement Mzize.

Hii ni mara ya pili kwa Nabi kutua nchini mwaka huu kwa mazungumzo na viongozi wa Yanga. Mapema Januari, kocha huyo alikuja lakini hakufanikisha mazungumzo yoyote, kwani Yanga haikuwa tayari kujadili mustakabali wa wachezaji hao nyota.

Mzize na Nabi wana historia ya kipekee. Ilikuwa chini ya uongozi wa Nabi ambapo Mzize alipandishwa katika kikosi cha kwanza, na mara kadhaa alitumiwa kama mshambuliaji wa akiba wa Fiston Mayele kabla ya Mayele kujiunga na Pyramids ya Misri.

Kwa upande mwingine, Mzize amekuwa akivutia vilabu vikubwa barani Afrika, ikiwemo Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Hata hivyo, Yanga imeweka msimamo kwamba ofa yoyote itakayozingatiwa lazima iwe “nono” ili iwashawishi.

Kuhusu Djigui Diarra, anaendelea kuwa mhimili wa kikosi cha kwanza cha Yanga, huku akiwa na mkataba wa miaka miwili zaidi. Ingawa bado ni mchezaji muhimu, msemo wa soka unasema, “hakuna mchezaji asiye na bei” — jambo linalofanya mustakabali wake kubaki wazi.

Mashabiki wa Yanga sasa wanatazama kwa karibu mwenendo wa mazungumzo haya, huku wengi wakijiuliza: Je, Nabi atafanikiwa kuwarudisha watoto wake wa zamani upande wake? Au Yanga itasimama kidete kuwatunza nyota wake?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →