Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuskitishwa na umelaani vikali vitendo vya kupigwa, kuchaniwa jezi na kufukuzwa uwanjani kwa mashabiki wake katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa tarehe 25/05/2025 katika uwanja wa Amaan Zanzibar
Pamoja na kulaani vitendo hivyo, Yanga imewaasa mashabiki wake kuendelea kuwa waungwana, wasilipize kisasi na badala yake waendelee kuwakaribisha mashabiki wa timu nyingine katika mechi za Yanga ili kuendelea kufurahia mchezo wa soka

ADVERTISE HERE