Kiungo Maxi Nzengeli msimu huu amekuwa bora zaidi katika kutengeneza nafasi za mabao kuliko kufunga
Katika orodha ya vinara wa kutoa pasi za mabao, Maxi anachuana na Pacome Zouzoua wote wakitoa pasi za usaidizi 9
Nyota hao wa Yanga wako nyuma ya Feisal Salum wa Azam Fc mwenye pasi 13 za usaidizi wa mabao
Anayeshika nafasi ya nne ni kiungo mshambuliaji wa Singida Black Stars Josephat Arthur mwenye asisti 8 sawa na Prince Dube ambaye amehusika katika mabao mengi zaidi katika kikosi cha Yanga akiwa pia amefunga mabao 13
Stephane Aziz Ki ambaye tayari amejiunga na Wydad Athletic, yuko katika orodha hiyo akiwa na asisti 7 huku pia akifunga mabao 9
Katika orodha hii umegundua nini Mwananchi...?

ADVERTISE HERE