Nyota wa Yanga Kennedy Musonda na Clatous Chama ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kwenye majukumu ya timu za Taifa
Zambia inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Sudan na Tunisia
Nyota wengine wa Yanga ambao wanakwenda kwenye majukumu ya timu za Taifa ni Duke Abuya (Kenya), Prince Dube (Zimbabwe) na Djigui Diarra (Mali)
Bado TFF haijaweka hadharani kikosi cha Stars ambacho huenda kikacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini
Pengine mabeki Dickson Job na Ibrahim Bacca, kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Clement Mzize watajumuishwa katika kikosi hicho
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto nae amekuwa katika kiwango bora katika mechi za karibuni hivyo haitakuwa ajabu akirejeshwa kwenye kikosi cha Stars
ADVERTISE HERE