Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika (ACA), Injinia Hersi Said, jana alihudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 62 tangu Umoja wa Afrika (AU), ulipoanzishwa.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo alikuwa ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Thabo Mbeki, Wageni wengine waliohudhuria ni Mawaziri mbalimbali, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Mabalozi wa Waafrika na nje ya Afrika.
Katika hafla hiyo, Eng. Hersi alipata nafasi ya kutoa hotuba iliyolenga kudumisha maendeleo na kufungua mipaka ya kibiashara ndani ya Umoja wa Afrika.
Aidha, Eng. Hersi alimpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara katika kuujenga Umoja wa Afrika hasa katika kufungua mipaka na Ushirikiano wa Kibiashara.
"The Future of Africa is not something we wait for, It’s something we build Together," Eng Hersi Said.