Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemtaka mlinda lango namba moja wa timu hiyo Youthe Rostand kuimarisha kiwango chake kama anataka kubaki kwenye kikosi chake.
Zahera amesema anavutiwa na umbo la mlinda lango huyo na alitegemea asiwe anafungwa mabao mepesi.
"Alipaswa kuwa kipa bora kutokana na umbo lake. Hastahili kuwa anafungwa mabao mepesi, nimemtaka afanyie kazi makosa yake," amesema.
Rostand amekuwa akilalamikiwa na mashabiki wa Yanga kwa kufungwa mabao mepesi hasa yatokanayo na krosi licha ya kuwa na kiwango kizuri kwa ujumla.
"Tatizo za Rostand ni udhaifu wake katika kucheza krosi na linachangiwa na kushindwa kupanga walinzi wake na kupelekea kufungwa mabao mepesi," amesema Shabani, mwanachama wa Yanga.
Yanga imeshindwa kupata huduma endelevu kutoka kwa mlinda lango wake mwingine mwenye uzoefu Benno Kakolanya ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu huku mara kwa mara akiingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga kutokana na madai yake ya fedha za usajili.
Kwa sasa yuko katika kikosi cha Yanga mkoani Morogoro kinachotarajiwa kuivaa Mtibwa Sugar leo.
Kakolanya pia alidaka kwenye mchezo dhidi ya Prisons.

ADVERTISE HERE