Siku chache baada ya kuondoka Yanga na kujiunga Wydad AC ya Morocco, kiungo Stephane Aziz KI ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso kwa ajili ya michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki itakayochezwa mapema mwezi ujao
Burkina Faso itacheza ugenini dhidi ya Tunisia Juni 2 na siku nne baadae itacheza tena ugenini dhidi ya Zimbabwe
Aziz Ki ameanza kutambulishwa kama mchezaji wa Wydad CA aliyojiunga nayo mwanzoni mwa wiki hii akitokea klabu ya Yanga
Kinachosubiriwa ni uongozi wa Yanga kutoa taarifa rasmi ya kuondoka kwa MVP huyo wa ligi kuu ya NBC msimu uliopita

ADVERTISE HERE