Chama uhakika sasa kikosi cha kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2025
Chama uhakika sasa kikosi cha kwanza

Baada ya kuondoka kwa Stephane Aziz Ki kuelekea klabu ya Wydad Athletic kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, milango imefunguka kwa Clatous Chama kuchukua nafasi hiyo katika kikosi cha kwanza cha Yanga SC.

Hii ni fursa ambayo inaweza kurejesha hadhi ya Chama kama mmoja wa viungo bora zaidi nchini, hasa ukizingatia uzoefu wake mkubwa na uwezo wa kipekee wa kutengeneza nafasi na kufunga mabao.

Ukiwa ni msimu wake wa kwanza Yanga, Chama ametumika zaidi kama mchezaji wa akiba kutokana na uwepo wa Aziz Ki ambaye alikuwa katika kiwango cha juu

Ni wazi kwamba ilikuwa vigumu kwa kocha yeyote kumweka benchi Aziz Ki akiwa katika ubora wake. Hata hivyo, kila alipopata nafasi, Chama alionyesha thamani yake 

Sasa, pamoja na Pacome Zouzoua, Chama anabeba jukumu la kuhakikisha kuwa pengo la Aziz Ki halionekani sana. Wawili hawa wanatakiwa kuendeleza kazi ya kutengeneza nafasi na kufunga mabao katika mechi tatu muhimu zilizosalia — mbili za Ligi Kuu na fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Faida ya Kuwa na Chama Katika Kikosi

Chama ni kiungo mwenye ubunifu mkubwa, mwenye macho ya mbali uwanjani na anayeweza kusoma mchezo vizuri. Ana uwezo wa kupiga pasi za mwisho (final pass) kwa ustadi mkubwa, jambo linaloweza kusaidia mastraika wa Yanga Prince Dube na Clement Mzize kuendeleza kasi yao ya kuzifumania nyavu

Aidha, uzoefu wake katika mechi kubwa, unampa uwezo wa kutuliza mchezo na kuongoza mashambulizi wakati wa presha. Huu ni wakati wake wa kudhihirisha kuwa bado ana mengi ya kutoa.

Ni muhimu pia kutambua mchango wa Pacome Zouzoua ambaye msimu huu amekuwa katika kiwango bora zaidi hata kuliko Aziz Ki kwa upande wa mabao na asisti. Mshikamano kati ya Chama na Zouzoua unaweza kuwa silaha kubwa kwa Yanga katika mechi zilizosalia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’